Arsenal bado ngangari

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal wamekuwa wakionyesha mchezo mzuri sana tangu ligi kuanza

Arsenal jana usiku wamefanikiwa kurejea katika nafasi yao ya kwanza kwenye ligi ya Premier baada ya kuicharaza Aston Villa mabao mawili kwa moja.

Gunners waliwapiku Manchester City na Chelsea na kurejea juu ya orodha.

Ulikuwa ushindi rahisi kwa Arsenal kutokana na mabao ya Jack Wilshere na Olivier Giroud ndani ya dakika moja wakati wa kipindi cha kwanza . Bila shaka Arsene Wenger alikuwa mwingi wa furaha.

Villa muda wote walionekana tu kukimbiza vivuli vya wachezaji wa Arsenal ingawa hatimaye walifanikiwa kuingiza bao la kichwa kupitia kwa Christian Benteke na kuzua wasiwasi kwa watani wao

Gunners walipata ushindi waliostahiki huku wakizidisha idadi ya mechi walizoshinda hadi mechi 15 tangu mwaka 1998.

Na kulikuwa na habari zaidi njema, ingawa mwanzo Theo Walcott hatacheza tena msimu huu naye mchezaji mwengine Alex Oxlade-Chamberlain amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu.