Murray asonga mbele Australian Open

Image caption Murray angali anapona kutokana na upasuaji aliofanyiwa mgongoni

Mchezaji wa Tennis Andy Murray ameonyesha wazi kuwa na yeye yumo mbioni kuwania ubingwa wa mashidnano ya tennis ya Australian Open baada ya kumbwaga Feliciano Lopez katika raundi ya tatu ya mashindano hayo yanayoendelea nchini Australia.

Muingereza huyo akicheza kwenye mashindano yake ya pili tangu kufanyiwa upasuaji , alishinda seti zake zote kwa poiti 7-6 (7-2) 6-4 6-2 katika ukumbi wa Hisense na kuwa miongoni mwa wachezaji bora kumi na sita.

Katika mechi itakayofuata, Murray atapambana na Stephane Robert.

Murray, mwenye umri wa miaka 26, atacheza mechi hiyo wengi wakiwa wanamuunga mkono aweze kushinda. Hata hivyo amepuuza nafasi yake ya kuweza kushinda taji lengine Jumapili ijayo.

"nimeweza kupona vyema, baada ya mechi zote,'' alisema Murray. '' mara kwa mara mimi husikia uchungu lakini kwa ukubwa sina matatizo sana.''

Kusinda mechi mbili mfululizo, katika ufunguzi wa mashindano hayo, ni jambo la kumtia motisha Lopez.

Lopez, mwenye umri wa miaka 32, alimpa Murray mazoezi wakati wa mechi yao ya kwanza katika joto kali la nyuzo 20 ikilinganishwa na nyuzi joto 40 za siku za kwanza za michuano hiyo.