Cavani na Suarez ndio tegemeo Uruguay

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Luiz Suarez

Miaka imebadilika na kuwa miezi na sasa ni miezi nne pekee , kabla ya mashindano ya kombe la dunia huko Brazil kuanza.

Makocha wanaendelea na maandalizi kuhakikisha timu zao zimekamilika idara zote ima ni safu ya ushambulizi ,ya kati na safu ya ulinzi kabla ya kipenga cha kuanza kwa kombe la dunia .

Kulingana na tafiti za ushabiki ,kombe la dunia ndilo lenya ufuasi mkubwa zaidi kote duniani .

Haki miliki ya picha
Image caption Edison Cavani

Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez , amesema kuwa washambulizi wa timu hiyo Luis Suarez na Edinson Cavani wapo katika umri bora wa kushamiri katika kinyanganyiro cha Kombe la dunia huko Brazil.

Tabarez anamatumaini kuwa kuwa washambulizi wake wanaujuzi na uwezo wa kutwaa kombe hilo baada ya kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali katika kombe la duna la 2010.

Uruguay ambayo imewahi kushinda kombe hilo mara mbili iko katika kundi D na Costa Rica, Uingereza, Italia na wenyeji Brazil.