Adebayor aendelea kutokomeza vilabu

Image caption Emmanuel Adebayor

Emmanuel Adebayor kwa mara nyingine tena aliifungia Tottenham Hotspurs bao muhimu lililoisaidia kujizolea alama tatu muhimu, na kuimarisha nafasi yake ya kushiriki katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, alinufaika na mkwaju wa adhabu uliopigwa haraka haraka ambao kipa wa Newcastle Tim Howard hakuuona.

Kufuatia ushindi huo Tottenham sasa imepanda hadi nafasi ya tano kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier huku Everton ikishuka hadio nafasi ya sita.

Vijana hao wa Roberto Martinez hata hivyo wamelalamika kuwa refa wa mechi hiyo aliwanyima penalti baada ya Seamus Coleman kufanyiwa madhambi na Etienne Capoue wakati wa muda wa ziada.

Ushindi huo unaendelea rekodi nzuri ya kocha mpya wa Tottenham, Tim Sherwood.

Tangua kuteuliwa kocha wa Spurs, Sherwood ameshinda mechi sita kati ya tsia alizoziongoza na amesema ushindi huo umetokana na juhudi za adebayor ambaye alikuwa ametengwa na kocha wa zamani Andre Villas-Boaz.

Kwa upande wake Everton, ambayo haikuwa na nyota wake Romelu Lukaku, ambaye anauguza jeraha, imefungwa magoli katika mechi tisa kati ya kumi zilizopita za ligi kuu.