Liverpool yalalamika kunyimwa Penalti

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers

Kocha Brendan Rodgers wa Liverpool amemlalamika Mwamuzi wa mechi ya jana dhidi ya Arsenal Howard Webb kwa kuwanyima Penalt ambayo kocha huyo anadai kuwa ilikuwa ya wazi Zaidi katika mechia mbayo Liverpool walilala kwa bao 2-1 na hivyo kutolewa katika Michuano ya kuwania Kombe la FA nchini England.

Kocha huyo amenukuliwa kuwa ulikuwa uamuzi wa kushangaza pale Mwamuzi Howard Webb alipokaa kuwapa Penalt ambayo ingekuwa ya pili baada ya mshambuliaji wao Luis Suarez kuchezewa madhambi na Alex Oxlade Chamberlain ndani ya eneo la hatari lakini mwamuzi ambaye alikuwa karibu kabisa na eneo la tukio akashindwa kutoa adhabu.

Awali Mwamuzi huyo ambaye atakuwepo Brazil baadae mwezi June mwaka huu kwenye Fainali za kombe la Dunia alitoa adhabu ya Penalt dhidi ya Arsenal katika dakika ya 59 baada ya Lucas Podolski kumchezea madhambi Suarez ambapo Steven Gerrard alitia kimiani Penalt hiyo kiufundi,Lakini dakika nane baada Luis Suarez tena akachezewa madhambi huku Mwamuzi akishindwa kutoa adhabu ambayo Kocha Brendan Rodgers anasema ilikuwa ya wazi Zaidi.

Kwa upande wake Kocha Arsene Wenger wa Arsenal anasema hana hakika kama tendo lile lilistahili kuwa Penalt,na kwamba angetizama baadae picha za marudio ili kuona kama ilistahili au la.

Katika Mechi hiyo ya Jana mlinda mlango Lucas Fabianski wa Arsenal alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo mikali kutoka kwa washambuliaji wa Liverpool Suarez,Sturridge na Coutinho ambao kwa nyakati tofauti walilitia msukosuko lango la Arsenal

"Nadhani Timu bora ndiyo imepoteza mchezo,hasa baada ya kutawala mchezo kwa kipindi kirefu nadhani tulistahili kupata kitu katika mechi hii,"alinukuliwa Kocha Brendan Rodgers.

Kwa matokeo hayo ya Jana Arsenal itakutana na Everton katika Robo Fainali,Huku Manchester City ikikabiliana wababe wake mwaka jana kwenye Fainali Timu ya Wigan Athletic.