Wahindi 500 walikufa Qatar

Image caption Wafanyikazi wa kigeni Qatar

Ripoti katika gazeti moja la Uingereza yasema zaidi ya raia wa India 500 walifariki wakati wakifanya kazi chini Qatar katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Ubalozi wa India nchini Qatar umesema vifo hivyo ni vya kawaida.

Awali Wizara ya leba ya Qatar ilisema takwimu hizo huenda zinajumlisha waliofariki kwa sababu za kibinadamu , ajali kazini na barabarani.

Wakekeretwa wanaamini nyingi ya ajali hizo zilifanyika katika kazi za ujenzi wa miradi inayohusiana na kombe la dunia ambalo Qatari inatarajiwa kuliandaa 2022.

Shirika la kandanda duniani FIFA lilitoa mwongozo wa jinsi ya kudumisha haki za wafanyikazi wanaojenga muundo msingi na viwanja na kuwahimiza Qatar kuitilia maanani haki ya wafanyikazi.

Mapema mwezi huu ,Shirika la kupigania haki za binadamu lilisema kuwa takriban watu mia mbili walikufa nchini Qatar na kuilazimisha shirikisho la soka Duniani FIFA kuingilia kati kuilazimisha serikali ya nchini hiyo kuandaa mufaka mpya wa wafanyikazi.