Mchezaji mkongwe Mario Coluna afariki

Image caption Mario Coluna

Aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya Benfica kutoka Msumbiji Mario Coluna amefariki nchini Msumbuji akiwa na umri wa miaka sabini na nane.

Coluna aliongoza timu ya Benfica kushinda mataji kadhaa barani ulaya na vile vile aliichezea timu ya taifa ya ureno katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 1966.

Alipostaafu Coluna alirejea nyumbani ambako alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Msumbiji.

Serikali ya Msumbiji imetangaza kua Coluna atapewa mazishi ya heshima zote za kitaifa.

Kifo chake kimetokea mwezi mmoja baada ya kifo cha mwanakandanda mwengine mashuhuri wa Msumbiji Eusebio aliyefariki nchini Ureno.