Andy Murray ashindwa Indiana Wells

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray

Baada ya Arsenal na Manchester City kubanduliwa nje ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya, masaibu ya wachezaji wa uingereza yanazidi kuendelea.

Muingereza Andy Murray ambaye ni bingwa wa mashindano ya Tennis ya Wimbledon naye ameondolewa katika raundi ya nne mashindano ya tennis ya BNP Paribas yanayoendelea, mjini Indiana Wells, Carlifonia.

Murray alishindwa kwa seti tatu kwa moja na Milos Raonic ambaye ameorodheshwa kama mchezaji wa kumi bora katika mashindano hayo.

Raonic, kutoka Canada mwenye umri wa miaka 23, amefuzu kwa robo fainali ya mashindano kufuatia ushinda wake wa seti tatu kwa moja za 4-6 7-5 6-3.

Murray alionekana kuchanganyikiwa katika seti ya pili, na kwa wakati mmoja alizozana na refa wa mechi hiyo kuhusu mahala ambapo camera ya video inapaswa kuwekwa.

Baada ya mech hiyo Murray alikiri kuwa hakuwa na anajiaamini na alikuwa na wasi wasi kuhusu hali yake baada ya kupoteza nafasi mbili za wazi ambazo zilifanya mpinzani wake kumshinda.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Milos Raonic ambaye alimshinda Andy Murray