Man City 1 Hull City 0

Image caption City yaibwaga Hull bao moja bila

Klabu ya Manchester City ilijikwamua baada ya bao lao kukataliwa na refa katika mechi yao dhidi ya Hull City Jumamosi.

Baada ya mechi hiyo walifanikiwa kurejea katika nafasi ya pili katika jedwali la idadi ya mabao za vilabu katika ligi ya Premier.

Kinara wa klabu hiyo, Kompany alipata kadi nyekundu baada ya kumuangusha Nikica Jelavic alipokuwa anakimbia kuelekea katika lango.

Lakini mkwaju wa David Silva uliwaondoa wasiwasi Man City na nusura mkwaju mwingine wa Pablo Zabaleta kuingia langoni na kuongeza idadi ya mabao ingawa hilo halikufaulu.

Tigers walimiliki mpira kwa kipindi kirefu lakini hawakupata nafasi nyingi za kuingiza mabao na Edin Dzeko ndiye alifanikiwa kuingizia Man City bao la kutuliza moyo na kupanda jedwali huku mechi ikikamilika kwa bao moja bila