Arsenal yailaza Tottenham Spurs 1-0

Image caption Tomas Rosicky ndiye aliingiza bao la uokozi kwa Arsenal

Klabu ya Arsenal leo imeimarisha ari yake ya kutaka sana kushinda kombe la ligi kuu ya Premier kutokana na bao la pekee la Tomas Rosicky ambalo limeinua zaidi matumaini ya Gunners dhidi ya Tottenham.

Rosicky aliingiza bao lake dakika chache tu baada ya mchezo kung'oa nanga.

Mchezaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor alijaribu bahati ya kuingiza bao katika kipindi cha kwanza Tottenham ikiwa imedhibiti mchezo ingawa hakufua dafu.

Mkwaju wake Nacer Chadli ulizuiwa kwenye msitari wa lango huku mkwaju wake Adebayor ukiwa umepoteza mwelekeo sana lakini Arsenal hawakuishiwa matumaini.

Ushindi huu una maana kuwa Arsenal wanashikilia nafasi ya tatu katika jedwali la alama lakini wakiwa nyuma ya kiongozi Chelsea kwa alama nne.

Chelsea walishindwa bao moja Bila na Aston Villa katika mechi yao.