Droo ya ligi kuu ya mabingwa ni leo

Haki miliki ya picha
Image caption Droo ya CL kufanyika leo

Droo ya robo fainali ya kombe la mabingwa Uropa itafanyika baadaye leo.

Timu nane, Manchester United na Chelsea kutoka Uingereza ziatakuwa zikitarajia upinzani mkali ikikumbukwa kuwa

mabingwa watetezi Bayern Munich walikutana na timu mwenza ya Ujerumani,Borussia Dortmund katika fainali za mwaka

uliopita. Lakini dakika tisini ndiyo itakayoamua mbivu na mbichi kwani kutakuwa na upinzani mkali kutoka vinara wa ligi kuu ya

Uhispania Real Madrid Barcelona bila kuisahau Athletico Madrid zote hizo zinazoshikilia nafasi tatu za kwanza katika ligi

yao ya nyumbani la Liga.

Timu nyengine itakayosubiri kujua itachuana na nani ni Paris Saint Germain kutoka Ufaransa.

Mbali na timu hizo kushikilia nafasi nane bora miongoni mwa vilabu bara Uropa wadadisi wengi wa maswala ya kandanda

wanaipigia upatu Bayern Munich kuhifadhi taji lao.

Licha ya kushindwa katika fainali msimu uliopita Borussia Dortmund na Manchester United ndizo zinaosemekana kuwa

timu dhaifu kutokana na hali ilivyo katika ligi zao za nyubmani.

United imekuwa msururu wa matokeo duni katika ligi ya Uingereza na inashikilia nafasi ya Saba.