Arsenal yaadhibiwa vikali na Chelsea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mohamed Salah

Arsenal walipata kichapo cha mwaka tena wakiwa wamesalia wachezaji 10 uwanjani, Mvua ya mambo ilinyesha huku Arsenal wakipata kichapo cha mabao 6-0.

Hiyo ndiyo adhabu Chelsea iliamua hii leo kuipa Arsenal.

Arsenal walichapwa mabao mawili katika dakika za kwanza saba za mechi, bao la kwanza likiingizwa na Samuel Eto'o likifuatiwa na la pili kutoka kwa Andre Schurrle.

Penalti ya Eden Hazard baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kugusa mpira kwa mkono ilikuwa dalili ya Arsenal kuvunjika matumaini.

Oscar aliingiza mabao mawili kabla ya Mohamed Salah kutonesha kidonda cha Arsenal.

Mkwaju wa Salah ndio ulikamilisha mchana wa majonzi kwa Arsenal. Mabao yalikuwa yamefika sita bila ya jibu lolote kutoka kwa Arsenal.

Kieran Gibbs alipewa kadi nyekundu kimakosa.

Huu ulikuwa ushindi mkubwa zaidi kwa Jose Mourinho katika ligi ya Premier na pia ni mara ya kwanza katika historia ya Chelsea kuingiza mabao sita dhidi ya mahasimu wao mjini London.

Chelsea wapata penalti baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kumtendea madhambi Eden Hazard, lakini Gibbs akapata kadi nyekundu kimakosa.

Yote haya yamefanyika katika wiki ambapo Wenger amepata sifa kwa kazi yake nzuri katika klabu ya Arsenal. Wenger alisema kila kichapo kinauma sana.