Man U yakoseshwa amani nyumbani

Image caption Kocha wa Man U David Moyes

Manchester City iliendelea kujiimarisha na kuikosesha amani klabu ya Manchester United katika ligi kuu ya premier.

Sio hilo tu bali Man City wanaongeza shinikizo kali kwa Chelsea walio juu kwenye jedwali la ponti katika ligi hiyo.

Man Uinted walipata kichapo cha mbwa cha mabao matatu bila nyumbani Old Trafford.

Edin Dzeko aliingiza mabao mawili katika kila kipindi kwa City hapo jana huku Yaya Toure akizidisha machungu kwa bao la tatu mwishoni mwa mechi bila jibu kutoka kwa Man United.

Sasa vijana hao wa City wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.