Durban au Edmonton 2022?

Image caption Wanamichezo wa Commonwealth katika ufunguzi

Mji wa Durban nchini Afrika Kusini na Edmonton nchini Canada imeonyesha nia ya kutaka kuandaa michezo ya Jumuia ya Madola, Commonwealth ya mwaka 2022.

Afrika Kusini haijawahi kuandaa michezo hiyo hapo kabla, wakati ambapo mji wa Edmonton uliandaa michezo hiyo mwaka 1978.

Miji inayowania kuandaa michezo ya 22 ya Commonwealth lazima ithibitishe ifikapo Marchi 2015, ambapo miezi sita baadaye Shirikisho la Michezo ya Commonwealth,CGF litayapitia maombi hayo.

CGF imekuwa na wasiwasi kuhusu nchi 70 wanachama kutoonyesha nia ya kutaka kuandaa michezo hiyo siku za baadaye.

Nchi wanachama wamepewa nafasi hadi Jumatatu kuonyesha nia ya kuomba rasmi kuandaa michezo ya baadaye.

Rais wa CGF Tunku Imran amesema nia ya miji ya Durban na Edmonton ni mwelekeo mzuri kwa michezo hiyo kusonga mbele na kuiongezea nguvu michezo hiyo duniani.".

Michezo ya 20 inaanza katika mji wa Glasgow JUlai 23 mwaka huu, huku mji wa Gold Coast nchini Australia ukijiandaa kuwa mwenyeji wa michezo ya mwaka 2018.