Mashabiki wamtaka Wenger astaafu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wamtaka Wenger aondoke

Arsene Wenger aendelee au asiendelee?

Ndio wimbo unaorindima ndani ya mioyo ya mashabiki wa Arsenal.

Hii ni baada ya kuchapwa 3 na Everton jana.

Mashabiki wanamlaumu Wenger naye Wenger mwenyewe anakilaumu kikosi chake.

"Lililobaki kwa silimia 100 tutang'ang'ania nafasi ya nne ingawaje ni vigumu," Wenger amesema.

Wenger ambaye amehudumu katika wadhfa huo katika mechi 1003 amewahi kuingoza timu hiyo ya Uingereza kufuzu kwa mashindano 16 ya kombe la mabingwa barani Ulaya.

Shabiki mmoja auliza katika mtandao wa twitter kuwa iweje January walikuwa nambari moja, february nambari 2, Mwezi wa tatu 3 na sasa mwezi wa nne nambari nne?

Mwingine asema Bwana Wenger amemtetea kwa miaka mingi - tisa kwa idadi -lakini leo amekoma.

Amejiunga na wale ambao wameanzisha kampeni katika mtandao Wenger ajiuzulu.

Kilio cha Arsenal ni furaha ya Liverpool ambao baada ya kuitandika West ham 2-1 wametuliza kileleni mwa ligi

Bashasha sasa pia zasikika katika kambi iliyokuwa imefifia ya Manchester United baada ya kuimwagia machungu yao yote Newcastle 4- 0 .

Kutokana na Ushindi huo Vijana wa David Moyes hatimaye wameimarika kutoka nafasi ya 7 hadi nambari 6.