Mourinho ampa kongole refa Dean

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jose Mourinho alikataa kuhojiwa na wanahabari baada ya Chelsea kushindwa

Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, alikataa kuhojiwa baada ya mechi kati ya klabu yake na Sunderland ambapo Chelsea walishindwa kwa mabao mawili kwa moja Jumamosi

Badala yake Mourinho alimpa kongole refa wa mechi hiyo Mike Dean na mkuu wa marefa Mike Riley baada ya kusifu vilabu hivyo viwili kwa walivyocheza.

Penalti iliyozua utata imesababisha Chelsea kuwa nyuma kwa pointi mbili dhidi ya viongozi wa ligi Liverpool.

''Uamuzi wake ulikuwa mzuri sana,'' alisema Mourinho kumhusu refa Dean.

Ushindi mkubwa wa Sunderland dhidi ya klabu kubwa ya Chelsea umevunja matumaini ya klabu hiyo kushinda ubingwa wa ligi ya premia.

Hatua ya kushindwa kwa Chelsea kunawapa matumaini Liverpool kusalia mbele na nafasi nzuri ya kutwaa taji.

Mourinho alilazimika kumzuia naibu wake Rui Faria kukabiliana na refa ambaye aliwapa Sunderland penalti katika dakika ya 79 ambapo Fabio Borini aliingiza bao na kuwapa ushindi Sunderland.

Alimpongeza refa akisema kuwa wakati mwingine ambapo marefa wanaendesha mechi vyema ni vizuri kuwapongeza.

"Mike Dean aliendesha mchezo huo vyema sana wakati marefa wanapofanya kazi nzuri ni vizuri kuwapongeza,'' alisema Morinhio

"alikuja hapa kwa nia moja, kuendesha mchezo vizuri na alifanikiwa kufanya hivyo. Hongera sana Mike Riley,kwa sababu marefa wamefanya kazi nzuri msimu huu,'' alisema Mourinho