Liverpool yakaribia ushindi wa ligi

Haki miliki ya picha All Sport

Liverpool ndio washindi watarajiwa wa ligi ya Uingereza baada ya Kuishinda Norwich City mabao matatu kwa mbili katika mechi iliyochezwa wikendi.

Kwa sasa Timu ya Liverpool iko na pointi tano zaidi, wakiwa wangali wana mechi kadhaa za kucheza ikiwemo ile ya Chelsea.

Japo Chelsea wamesalia katika nafasi ya pili walishindwa kujiimarisha hapo jumapili na kusababisha kuwepo kwa mwanya huo mkubwa baada ya kushindwa na timu ya Sunderland kwa mabao mawili dhidi ya lao moja.

Timu ya Sunderland ndio iliyo ya mwisho kabisa katika orodha.

Ilimbidi mkufunzi wa Chelsea Jose Mourihno kuipongeza Sunderland pamoja na refa aliyeendesha mechi ile ingawa kwa kinaya kwani ilikuwa ni kama kumtoneshea kidonda hasa baada ya ile faini aliyopigwa baada ya kupatikana na kosa la kumkaripia refa katika mechi ambapo alihisi ameonewa.