Chelsea na Atletico sare tasa UEFA

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Paul Garcia wa Atletico Madrid (kushoto) na mwenzake Diego wanang'ang'ania mpira na wachezaji wa Chelsea 22.04.14 katika nusu fainali ya UEFA 2014.

Kwa kulinda lango Chelsea walicheza mechi yao ya nusu fainali ya Champions league jana usiku huku wakiwanyima kila fursa ya kufunga wapinzani wao Atletico Madrid na kulazimisha sare tasa.

Wengi wa mashabiki wa klabu hiyo inayoshikilia nambari mbili katika ligi ya nyumbani walishusha pumzi za afueni kwani walikuwa na kila sababu za kuiogopa Atletico Madrid timu sugu, huku upande wao wakikabiliwa na majeraha ya wachezaji wake muhimu akiwemo mlinda lango.

Hata hivyo itambidi meneja Jose Morihno kutafuta mbinu nyengine ya kimuijiza ndio waruke kizingiti cha raundi ya pili nyumbani Stamford Bridge hapo wiki ijayo. Mshindi wa mechi hiyo atakutana na Real Madrid au Bayern katika fainali.

Nahodha wa Chelsea John Terry pia atakosa mechi iliyosalia ya msimu huu wa league ya premier kutokana na jeraha alilopata jana - mechi nyeti dhidi ya kiongozi wa ligi hiyo Liverpool hapo jumapili.

Msimu wa ligi ya Premium unaisha katika kumi la kwanza la Mei huku fainali ya EUFA ikipangiwa mwishoni mwa Mei. Huku Chelsea ikiwa timu ya pekee katika Champions League Murihno amesema yeye na kokosi chake wataelekeza nguvu zao zote katika kinyanganyiro hicho.

Huku vilabu vingi vikubwa vikijishughulisha na jinsi watakavyokamilisha msimu , Manchester United imejikuta kwenye mapana na marefu ya kumtafuta kocha mpya baada David Moyez kutimuliwa.

Jinsi msimu ulivyowaendea vibaya hadi mahesabu ya kupata nafasi ya ushirika katika champions league msimu unaokuja kuborongeka, kitendo hicho pekee cha kumfuta kazi Moyez angalau kimepandisha hisa za klabu hiyo tajiri kwa asilimia 6, kiwango imara kurekodiwa tangu Mei mwaka jana. .

Japo wenye klabu wamemuweka mchezaji veterani Ryan Giggs kusimamia klabu hiyo kwa mda, swali ni mbinu gani itatumiwa kumtafuta msimamizi wa kudumu wa klabu hicho baada uamuzi wa awali wa mumwachia Sir Alex Fergerson kuchagua mrithi wake kwenda mrama..? .