Fainali na Real ni Chelsea au Atletico?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption John Terry nahodha wa Chelsea

Nahodha wa Chelsea John Terry na Eden Hazard watakuwa tayari katika kikosi cha Jose Mourinho kitakachocheza dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa marudiano hatua ya nusu fainali ya Kombe la UEFA mjini London, Jumatano.

Hata hivyo mlinda mlango tegemeo wa Chelsea, Petr Cech hatajumuishwa kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa majeruhi.

Terry aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa kutofunganauku Cech akiteguka bega.Mark Schwarzer ambaye amekuwa akifanya vizuri langoni tangu kuumia kwa Cech ataendelea kulilinda lango la Chelsea.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Atletico Madrid wakifurahia goli

Hazard, atacheza kwa mara ya kwanza tangu Aprili 8 na Samuel Eto'o naye ni imara kuweza kucheza mchezo huo.

Nahodha wa Atletico Gabi anatumikia adhabu ya kadi, ambapo mchezaji kiungo wa zamani wa Chelsea Tiago Mendes anatarajiwa kuchukua nafasi yake.

Swali linalobaki ni nani kati ya Chelsea na Atletico atakayeungana na Real Madrid kucheza fainali ya UEFA mwaka 2014 mjini Lisbon? Real imefuzu kucheza fainali za UEFA mwaka huu baada ya kuisambaratisha Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-0 na hivyo kuivua rasmi ubingwa na kuliacha kombe hilo likiwaniwa na timu mpya.