Mabondia wa Kenya wang'ara Sri Lanka

Image caption Rayton Okwiri (kushoto) alishinda medali ya dhahabu

Mabondia wa Kenya wamezoa medali tatu katika mashindano ya Ndondi ya Lions Cup yaliyomalizika leo nchini Sri Lanka.

Walioshinda medali hizo ni Rayton Okwiri dhahabu uzani wa Walter, Dennis Okoth Fedha uzani wa light Welter na Simon Mlinge aliyezoa shaba katika uzani wa Fly.

Habari hizi ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha ndondi cha Kenya John Kameta.