Giggs asema hasikitishwi kamwe

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kaimu mkufunzi wa timu ya Manchester United Ryan Giggs

Kaimu mkufunzi wa timu ya Manchester United nchini Uingereza, Ryan Giggs amesema kuwa hasikitishwi na hatua ya kumtafuta kocha mpya wa kilabu hiyo .

Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal ambaye anaitaka kazi hiyo anatarajiwa kuteuliwa kama mrithi wa aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo David Moyes.

Giggs aliteuliwa kama kaimu kocha wa kilabu ya Manchester United baada ya Moyes kutimuliwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya mnamo mwezi Aprili.

Wakati huohuo mshambulizi wa kilabu ya Manchester United Wayne Rooney yuko tayari kuonyesha uhodari wake katika michuano ya kombe la dunia.

Kulinga na kaimu meneja wa kilabu yake Ryan Giggs,Rooney ameshindwa kung'ara katika michuano mingi ya kimataifa tangu alipoanza kusakata soka ya kiwango hicho katika mechi za kuwania taji la ubingwa wa ulaya mnamo mwaka 2004.

Hatahivyo Giggs ana imani kwamba Rooney ataiwakilisha vyema Uingereza katika dimba la dunia nchini Brazil.