Mmiliki wa clippers aomba radhi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa timu ya Clippers wakijiandaa kwa mechi

Mmiliki wa klabu ya mpira wa vikapu ya Los Angeles Clippers, Donald Sterling, ameomba radhi kwa matamshi yake ya kibaguzi.

Shirikisho la mchezo huo nchini Marekani lilimpiga marufuku maisha.

Bwana Sterling aliambia kituo cha televisheni cha American TV kuwa alifanya kosa kubwa sana ambalo hata hajui anavyoweza kulirekebisha.

Katika mahojiano yatakayopeperushwa leo, itakuwa kauli ya kwanza ya Sterling tangu kutokea kakanda nambayo alikuwa anamkarpia mpenzi wake kumtaka akome kujihusisha na watu weusi.