Atletico Madrid Mabingwa wa La Liga

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia goli

Atletico Madrid imenyakua kombe la ligi kuu ya Hispania La liga baada ya kutoka sare ya 1 – 1 dhidi ya Barcelona na hivyo kumaliza ligi ikiwa na pointi 90 huku Barcelona ikishika nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 87.

Real Madrid iliyoshinda mechi yake dhidi ya Espanyol kwa 3 - 1 ikishika nafasi ya tatu kwa kumaliza ligi ikiwa na pointi 87 lakini ikizidiwa na Barcelona kwa tofauti ya goli moja.

Barcelona wana tofauti ya magoli 67 wakati Real Madrid ikiwa na tofauti ya magoli 66.

Katika mechi hiyo ya Barcelona dhidi Atletico Madrid ambayo ilikuwa ni ya kuamua ni timu ipi itanyakua ubigwa wa La Liga msimu huu, Barcelona ndio waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu wa Atletico Madrid kwa goli lililofungwa na Alexis Sanchez katika ya 34 kipindi cha kwanza.

Baadae Atletico Madrid walikuja juu na kuanza kulishambulia goli la Barcelona ambapo Diego Godin katika dakika ya 49 kipindi cha pili aliIsawazishia timu yake kwa goli safi alilolipachikwa wavuni kwa njia ya kichwa na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike kwa jumla ya goli 1 - 1 .

Atletico Madrid inakuwa mabingwa wa La Liga tangu baada ya kulikosa kombe hilo tangu mwaka 1996.