Arsenal - mabingwa wa kombe la FA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Arsenali yashinda FA

Sherehe za Arsenal zapamba moto London

Ukame umeisha --- ndio usemi ulio midomoni na mioyoni mwa mashabiki wa Arsenal baada ya wikendi ya nderemo na vifijo vya ushindi.

Wachezji wakiwa kwenye basi la wazi huku mashabiki unyounyo hapo jana wamepamba mitaa ya London kwa rangi zao nyekundu wakipokelewa kwa hadhi na bashasha kila walikopitia.

Arsenal 'the gunners' kweli wanatamba kwenye chati, mitandao ya kijamii na kwengineko. Arsene Wenger akionekana akinadi kombe hilo la FA waliloshinda baada ya kuinyuka Hull city 3-2.

Kombe lililosubiriwa kwa mda mrefu wa miaka 9. Hata wale waliokuwa na kampeni ya Wenger aondoke sasa wamegeuza wimbo kuwa mkataba wake uongezwe na fununu za hivi punde ni kuwa tayari ameshazawadiwa mkataba wa miaka 3 na kuwa kitita chamsubiri cha kununulia vipaji vipya vya wachezaji nyota duniani ili mavuno ya vikombe yaendelee.