UEFA yachunguza PSG kuhusu ubaguzi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption PSG yajipata matatani

UEFA imeanzisha uchunguzi wa PSG kuhusu madai ya ubaguzi wa rangi katika mchuano baina yao na Chelsea.

Timu ya Paris St Germain, imeitwa mbele ya kikao maalum cha kinidhamu cha UEFA, kuhusu shutuma za ubaguzi wa rangi, kitendo kilichofanywa na mashabiki wao, katika mechi baina ya timu hiyo na Chelsea, mwezi uliopita, huko Paris.

Shutuma hizo zinahusu ubaguzi wa rangi, tabia za kibaguzi na propaganda, katika mechi ya mkondo wa pili, ya robo fainali ya UEFA. PSG ilishinda mchuano huo, 3-1, lakini ikapoteza kwa sababu ya sheria ya mabao ya ugenini.

Taarifa ya UEFA, iliyotolewa kwa Press Asociation Sports, ilisema "Kesi ya kinidhamu, ilianzishwa dhidi ya PSG, mnamo 16 Mai 2014, kuhusiana na tuhuma hizo zinazohusu ubaguzi, na pia Propaganda, katika mchuano wao wa robo fainali na Chelsea huko Paris"

Tume ya uongozi na kinidhamu ya UEFA, itafanya uamuzi wake kuhusu kesi hiyo tarehe 17 Julai.

Mchuano huo ulikumbwa na vurugu baina ya mashabiki wa pande zote mbili katika barabara za Paris, huku mashabiki wa Chelsea wakisemekana kutoa matusi ya kibaguzi wa rangi na kuonesha ishara za Nazi, na kundi la takriban wafuasi 100 wa PSG, wakiwalenga mashabiki waliokua wakisafiri.

Ripoti katika tovuti ya gazeti moja la Paris; Le Parisien, Jumanne jioni, ilionesha kuwa kundi la mashabiki wasiojiweza wa Chelsea, walikua wametoa malalamishi baada ya kutupiwa taka kama vile chupa na peremende za kubugia wakati mchuano huo ukiendelea huko Parc Des Princes.

Sheria za kinidhamu za UEFA, zinabainisha kuwakiwango flani cha sehemu ya uwanja wao kufungwa, ikiwa watapatikana kuwa na hatia ya mashabiki wao kuwabagua kwa misingi ya rangi, mashabiki wa Chelsea.

Kitengo cha 14 cha sheria hizo pia kinasema: "kosa la pili litaadhibiwa kwa mchuano mmoja kuchezwa katika uga wao ukiwa umefungwa na bila mashabiki, na pia faini ya Euro 50,000.