Serena na Venus nje ya French Open

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwana-tennis mashuhuri Serena William hakung'ara katika mchuano wa mwaka huu.

Bingwa mtetezi wa French Open upande wa wanawake Serena Williams ameyaaga mashindano hayo, baada ya kunyamazishwa na Garbine Muguruza wa Uhispania kwa seti 6-2, 6-2.

Hii ni mara ya kwanza tangu Serena Williams kuanza kucheza mashindano hayo kuondolewa wiki ya kwanza ya mashindano.

Imekuwa pigo kubwa kwani dadake pia,Venus tayari alikuwa ameshaondolewa kutoka mashindano hayo ambayo yameingia siku ya nne sasa.

Venus alishindwa 2-6 6-3 6-4 na M-Slovakia Anna Schmiedlova.

Muguruza, mwenye umri wa mika 20, alimlemea gwiji huyo nambari moja Tennis ya wanawke aliyeonekana kufanya makosa madogo madogo lakini yakamgharimu sana.

Serena, Mmarekani mwenye umri wa miaka 32 amewahi kushinda taji hilo mara 17.

"Najihisi vibaya kuyaaga mashindano lakini mambo hayo hutokea wakati mwengine, ntajitahidi mara tano ya hivi leo wakati ujao' Serena alijiliwaza.

Mashabiki wake walishangaa kuona amezidiwa nguvu kinyume na kawaida yake,huku mpinzani wake akibaki mkakamavu na makini.

" Nilisi hakuwa sawa, na nkaona nna nafasi ya kushinda hapa,inanibidi nicheze vyema ndiyo nishinde! Amesema Muguruza ambae ameorodheshwa nambari 35 katika ulingo wa Tenis duniani.

Kwa miaka mingi dada hao wawili wameweza kutamba katika ulimwengu wa Tenis ya wanawake na Serena ndie mchezaji pekee mwanamke ambae amewahi kushinda zawadi ya zaidi ya $50 millioni kupitia Tenis.