Qatar kujibu masuali mbele ya FIFA

Haki miliki ya picha
Image caption fifa yaitisha uchunguzi kwa Qatar

Mchunguzaji aliyeteuliwa na Fifa , Michael Garcia hii leo atawahoji maafisa wa Qatar wanao simamia maandalizi ya Kombe la Dunia.

Naye rais wa UEFA, Michel Platini , amelilaumu gazeti la The Sunday Times kwa kumhusisha na kashfa hiyo ya Qatar.

Garcia atawachunguza kwa madai ya ufisadi katika kashfa inaozingira Qatar kupewa ruhusa ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka wa 2022.

Mapema wiki hii gazeti la Sunday Times kutoka Uingereza lilichapisha stakhabadhi zilozoonesha jinsi aliyekuwa afisa wa shirikisho la soka nchini Qatar Mohammed bin Hammam, aliwalipa mamilioni ya madola maafisa wa soka kwa ili kuiunga mkono Qatar kuandaa michuano hiyo mwaka mmoja kabla ya uamuzi kutolewa.

Michael Garcia amesema ripoti kamilifu katika uchunguzi huo utatolewa hapo mwezi ujao.