Mtu afariki ukuta ukiporomoka Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo la Monorail kulikoporomoka ukuta ukijengwa kwa Kombe la Dunia.

Mtu mmoja amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya sehemu iliyokuwa ikijengwa kuporomoka, katika harakati za kumalizia ujenzi muhimu wa eneo linaloitwa Monorail, taarifa kutoka Sao Paulo zimesema.

Ni eneo la kilomita 17 lililokuwa litumike kuunganisha uwanja wa ndege na mfumo wa usafiri wa reli mjini humo.

Brazil imekuwa ikisuasua na sasa inaharakisha kumalizia majengo na miundo mbinu iliyopangiwa kutumika wakati wa kombe la dunia.

Visa vya ajali kuhusiana na ujenzi huo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.

Wafanyikazi wanane walifariki wakati wa ujenzi wa eneo la katika la uwanja wa kombe la dunia 'arena'.