Wasio makaazi wasitisha mgomo Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa polisi wakimzuia mwandamanaji nchini Brazil

Vuguvugu la watu wasio na makaazi nchini Brazil ambalo limekuwa likiunga mkono maandamano ya kupinga kombe la dunia sasa wametangaza kuwa wamesitisha maandamano hayo muda wote wa dimba hilo.

Hii ni baada ya kufanikiwa kupata makubaliano na serikali, hata hivyo bado kuna wasiwasi kwa kuchipuza tena kwa mgomo wa wafanyakazi wa usafiri wa reli wa mjini uitwao 'Metro' ambao hawajapata uelewano na serikalii na wametishia kugoma tena kesho hadi pale madai yao ya nyongeza ya mshahara kwa 12% yatakapotekelezwa.

Kama kweli wakiendeleza vitisho hivyo basi itakuwa kasheshe kubwa mashabiki kusafiri hadi viwanjani kujionea mechi walizokuwa wakizisubiri kwa hamu kuu.

Mechi ya ufunguzi hapo kesho ni kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia.

Maandalizi ya kombe la dunia ya Brazil yamekubwa na chelewachelewa na pia migomo ya makundi mbalimbali yanayotumia fursa hiyo ya kombe la dunia kudai nyongeza za mishahara na huduma bora za kijamii kutoka kwa serikali inayoshtumiwa kwa ufisadi na matumizi makubwa katika ujenzi wa viwanja na miundo mbinu kwa ajili tu ya kombe la dunia.