Uingereza yanyamazishwa na Italy

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mario Balotteli Asherehekea bao lake la Ushindi

Mabingwa wa zamani wa kombe la dunia Italy wameanza vyema kampeni yake ya kuwania kombe la dunia nchini Brazil baada ya kuichapa Uingereza mabao mawili kwa moja katika mechi kali.

Bao la ushindi la Italy lilifungwa kwa kichwa kupitia mshambuliaji matata Mario Baloteli mda mchache tu baada ya kipindi cha mapumziko.

Awali mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge alikuwa amekomboa bao lililofungwa na Claudio Marchisio wa Italy.

Mechi hiyo ilichezwa chini ya viwango vya juu vya joto katika uwanja wa Manaus uliopo katikati ya msitu wa Amazon.

Katika mechi za awali ,Costa Rica ilitoka nyuma na kuishinda Uruguay mabao matatu kwa moja huku Colombia nayo ikiicharaza Ugiriki mabao matatu bila katika mji wa Belo Horizonte.

Wakati huohuo miamba ya soka barani afrika Ivory Coast imeimarisha matumaini ya bara hili baada ya kutoka nyuma na kuishinda Japan kwa mabao mawili kwa sufuri.

Ivory Coast ilijipatia mabao yake kupitia wachezaji Wilfried Bony na aliyekuwa mchezaji wa Arsena Gervinho huku Japan ikifunga kupitia mshambuliaji wake keisuke Honda.