Uingereza 1- 2 Uruguay

Haki miliki ya picha PA
Image caption Suarez ashangilia bao lake dhidi ya Uingereza

Mshambulizi wa Uruguay, Luis Suarez aliungata mkono unaomlisha alipofunga mabao mawili na kuisaidia Uruguay kasajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uingereza katika mchuano wao wa kundi D, huko Sao Paulo. Matokeo hayo yameiwacha Uingereza mguu nje mguu ndani ya kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil.

Hata ingawa mkufunzi wa Uingereza Roy Hodgson hakubadilisha kikosi chake kutokana na kile kilichocheza dhidi ya Italia huko Manaus katika mechi yao ya awali, alimpa Wayne Rooney nafasi ya kucheza katikati, nyuma ya mshambulizi Daniel Sturridge.

Kufwatia kichapo cha 3-1 dhidi ya Costa Rica, Oscar Tabarez alifanya mabadiliko 5 katika kikosi kilichochuana na Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Luiz Suarez 37''

Suarez aliyekua na jeraha la goti pia alijumuishwa katika kikosi hicho.

Suarez aliupiga mpira wa kona ambao ulimpata Hart akiwa hayuko tayari, hata hivyo aliweza kuutoa mpira huo nje na kusababisha kona nyingine. Nafasi nzuri ya Uingereza ya kupata bao, ilikuja pale Sturridge alipoupiga mpira ambao uligusa mkono wake Diego Godin naye refa wa mechihiyo Carlos Velasco akawapa waingereza mpira wa adhabu katikati ya ya uwanja.

Rooney aliupiga lakini ukatoka nje, hata ingawa hatua chache tu.

Timu zote mbili zilipata nafasi nzuri na umiliki , bila kukamilisha mashambulizi .

Hata hivyo Rooney alikaribia kufunga bao lake la kwanza katika michuano yote ya kombe la dunia ambayo ameshiriki katika dakika ya 31.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uingereza 0-0 Uruguay

Shuti yake Steven Gerrard iliingia katika eneo la penalti la Uruguay naye Rooney na Godin wakapigania mpira huo ambao Rooney aliupata kwa kichwa ila tu uligonga mwamba wa lango la Uruguay .

Nicolas Lodeiro aliupata mpira katikati ya uwanja na akampisha Edinson Cavani.

Mchezaji huyo wa Paris Saint Germain alimpiga chenga Phil Jagielka na akampata Suarez aliyefunga kwa kichwa.

Hayo, katika dakika ya 39, Suarez akawapa La Celeste, bao la kwanza.

Kama walivyofanya dhidi ya Italia, Uingereza pia ilishambulia muda mfupi baadaye. Rooney alimpa Sturridge pasi naye akawapita walinzi wa Uruguay na kutoa mkwaju uliookolewa na , kipa wa Uruguay Fernando Musclera.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suarez ashangilia bao lake dhidi ya Uingereza

Hata hivyo waingereza walikataa kufa moyo.

Dakika kumi na tano kabla mchuano kukamilika, Rooney alipata mpira kutoka kwa Glen Johnson naye akafunga bao la kusawazisha.

Bao lake la kwanza katika michuano yoyote ya kombe la dunia.

Timu zote mbili zilianza kutafuta bao la ushindi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa Uingereza walivumilia timu yao iliposhindwa na Uruguay

Mpira wake Musclera ulimfikia Suarez na mchezaji huyo wa Liverpool akaupita ulinzi wa Uingereza na kufunga bao la pili dhidi ya Hart zikiwa zimesalia dakika tano mechi kukamillika.

Uingereza bado ina matumaini ya kuendelea iwapo wataishinda timu ya Costa Rica na kusubiri ikiwa matokeo ya mechi baina ya Italia na Uruguay yatakuwa mazuri kwao.

Uingereza sasa watafurushwa kutoka kwenye kombe la dunia Brazil 2014 iwapo wapinzani wao katika kundi hilo Costa Rica watatoka sare ama kushinda Italia katika mechi yao ya pili itakayochezwa Ijumaa.

Matokeo :Uruguay wameilaza Uingereza 2-1

23:51 Mechi imekamilika

23:48 Uruguay 2-1 Uingereza

23:47 Dakika 5 za ziada.

23:45 Suarez anaondoka uwanjani zikiwa zimesalia dakika mbili mechi hii ikamilike .

23:43 Uruguay 2-1 Uingereza

23:43 Luiz Suarez anaifungia Uruguay bao la pili

23:32 Uruguay 1-1 Uingereza Rooney 75''

23:31 ROOOONEY !

23:31 Uingereza wanashambulia

23:26 Welbeck anaondoka anaingia Adam Lallana

23:24 Uruguay 1-0 Uingereza 70''

23:24 Steve Gerrard anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumwangusha Rodriguez

23:23 Nickolas Lodeiro anapumzishwa

23:20 Rooney anafanya mashambulizi lakini inakuwa bure Muslera anaupokea

23:20 Raheem Sterling anaondoka na nafasi yake inachukuliwa na Ross Barkley

23:15 Uruguay 1-0 Uingereza 60''

23:14 Ushirikiano baina ya Cavani na Luiz Suarez unawatatiza waingereza.

23:12 Kipa wa Uruguay Muslera anajeruhiwa na Muslera lakini Refarii anasema si hoja hiyo

23:10 Rooooooney anakosa nafasi nzuri akiwa amesalia na Muslera

23:09 Suarez anapiga tobwe lakini inatoka nje ni free kick.

23:04 Uingereza imenusurika kufungwa bao la pili kutokana kona ya Luiz Suarez

23:02 Luiz Suarez 37''

23:01 Uruguay bado inaongoza kwa bao moja kwa nunge.

23:00 Kipindi cha pili kimeanza bila ya mabadiliko yeyote kwa timu zote

22:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika Uruguay ikiongoza kutokana na bao la pekee la Luiz Suarez

22:45 Uruguay 1-0 Uingereza 45''

22:43 Uingereza inatafuta bao la kusawazishakwa udi na uvumba

22:42 Kona ya tatu kwa Uingereza .

22:40 Uruguay 1-0 Uingereza

22:39 Luiz Suarez 39''

22:38 Luiz Suarez anaiweka Uruguay mbele

22 :38GOOOOOOOAL

22:37 Uingereza 0-0 Uruguay 37''

22:36 Uruguay nayo lazima ishinde iwapo inataka kuendelea mbele na dimba hili

22:36 Uingereza inatafuta alama zitakazoinusuru aibu ya kubanduliwa nje ya kombe hili baada ya kulazwa 2-1 na Italia.

22:33 Freekick kuelekea lango la Uingereza inapigwa na Suarez

22:32 Uruguay 0-0 Uingereza 32

22:31 Rooney anapokea mkwaju wa Gerrard lakini unagonga mwamba na kurudi uwanjani.

22:30 Feekick kuelekea kwenye lango la Uruguay

22:26 Uingereza inapeana Kona ya tatu kwa Uruguay

22:25 Uingereza 0-0 Uruguay 25''

22:17 Sturridge anafyatua mkwaju unaokwenda nje na inakuwa ni Kona kuelekea lango la Uruguay.

22:17 Cristian Rodríguez Uruguay anatupa nje nafasi ya kufunga bao. Golkick.

22:10 Uruguay 0-0 Uingereza

22:09 Wayne Rooney ndiye anayeipiga Freekick

22:08 Diego Godin anaoneshwa kadi ya kwanza ya Njano nje ya eneo

22:07 Suarez anamenyana na mwenzake wa Liverpool Steve Gerrard

22:06 Freekick kuelekea upande wa Uruguay,,inadenguliwa

22:03 Luiz Suarez ndiye anayeipiga na inaondoshwa na kuwa kona ya pili

22:02 Kona ya kwanza ya mechi hii kuelekea lango la Uingereza

22:01 Kiti cha Tabarez kocha wa Uruguay kina misumari

22:01 Uingereza ikiongozwa na Dan Sturridge wanafanya mashambulizi ya mapema

22:00 Mechi imeanza

22:00 Uruguay inatafuta pointi ya kwanza katika kombe la dunia inapokabiliana na Uingereza.

21:58 Luiz Suarez anacheza katika mechi hii ambayo lazima Uruguay ishinde ilikufufua kampeini yake ya Kombe la Dunia

21:57 Hii ni mechi ya 23 ya kombe la dunia la Brazil 2014

Haki miliki ya picha Getty AFP
Image caption Uruguay inatafuta pointi ya kwanza katika kombe la dunia inapokabiliana na Uingereza.Timu zote zilishindwa katika mechi zao za ufunguzi.

21:56 Timu zote zilishindwa katika mechi zao za ufunguzi.

21:55 Uruguay inakabiliana na Uingereza katika mechi ya pili.