Japan yatoka sare na Greece

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Japan yatoka sare na Greece katika mechi ya mwisho

Japan na Ugiriki wamepata pointi zao za kwanza katika kombe la dunia Brazil mwaka 2014.

Matokeo haya yanaacha vikosi hivyo viwili vikiwa mwisho katika kundi C, vikiwa na alama moja.

Mechi hiyo ilichezwa katika uga wa Estsdios das Dunas, Natal.

Timu hizo mbili zilitoka sare bila kufangana bao lolote, huku Ugiriki ikimaliza mechi hiyo na wachezaji kumi baada ya nahodha wao kutimuliwa mchezoni.

Kundi lao laongozwa na Colombia na alama 6 nayo Ivory Coast ni ya pili kwa alama 3.

Mchezo mzuri katika mechi hii, kidogo ulionyeshwa na Japan.

Yuya Osaka alimjaribu kipa wa Ugiriki, Orestis Karnezis na mkwaju ambao ulitoka nje mapema mchezoni.

Keisuke Honda pia alipata nafasi katika dakika ya 29 alipopewa mpira wa adhabu yadi 25 kutoka lango la Ugiriki. Karnezis alizuia mkwaju huu pia.

Muda mfupi baadaye nahodha wa Ugiriki, Konstantinos Katsouranis, alionyeshwa kadi ya manjano kwa mara ya pili na akaondoka mchuanoni baada ya kumchezea vibaya nahodha wa Japan Makoto Hasebe.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Mashabiki wa Japan

Kuondolewa kwake kulitia moto katika kikosi cha Ugiriki na walionekana kuonyesha mchezo mzuri wakiwa wachezaji 10 kuliko walivyokua 11.

Vasileios Torosidis , alitoamwakju safi iliyomlakimu kipa wa Japan, Eiji Kawashima kufanya kazi ya ziada.

Georgios Samaras pia alijaribu bahati yake kutoka kwa mpira wa adhabu nao ukampita Kawashima ila tu ulielekea nje.

Kikosi hicho cha Fernando Santos kilizidi kushambulia na katika kipindi cha pili, Mchezaji wa akiba Theofanis Gekas aliugonga kwa kichwa mpira wa kona lakini ukaokolewa na kipa wa Japan.

Samurai Blue wa Japan waliamka pia katika dakika ya 68 pale ambapo Atsuto Uchida alipompa Yoshito Okubo mpira ila tu Okubo aliupiga nje.

Uchida pia akaijaribu safu ya ulinzi ya Ugiriki na mpira wake pia ukaelekea nje.

Japan ilimaliza mechi hiyo ikionekana kuwa yenye nguvu zaidi ya Ugiriki, Hata hivyo, ili kupata matumaini ya kuendelea, wanatarajiwa kukishinda kikosi cha Colombia kinachoongoza kundi hilo la sivyo ivory coast itamaliza katika nafasi ya pili.

Ivory coast imeratibiwa kuchuana na Ugiriki katika mechi yao ya mwisho ambayo ssa wanahitaji ushindi ilikujihakikishia nafasi ya pili nyuma ya Colombia ambayo tayaari imeshafuzu kwa mkondo ujao.