Raia wa Costa Rica washerehekea ushindi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mashabiki wa Costa Rika wakisherehekea

Makumi ya maelfu wa raia wa Costa Rica wamesherehekea ushindi wa timu yao ya taifa katika mechi za kombe la dunia zinazoendelea nchini Brazil baada ya kuishinda italy kwa bao moja kwa bila.

Raia hao waliokuwa wakipeperusha bendera walisherehekea ushindi huo ambao umewaweka katika nafasi nzuri ya kuingia katika awamu ya mchujo kwa mara pili

Ushindi huo pia unamaanisha kuwa Uingereza imebanduliwa nje ya mashindano hayo .

Wakati huohuo Ufaransa imepanda hadi katika nafasi ya kwanza ya kundi E baada ya kuicharaza Switzerland kwa mabao matano kwa mawili.

Katika mechi za kundi jengine Ecuador iliishinda Honduras kwa mabao mawili kwa moja katika mechi iliojaa msisimuko mkubwa.