Miraslov Klose afunga bao la 15

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa Ujerumani wakati wa mechi kati ya Ghana na Ujerumani

Mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose amefikisha idadi sawa ya mabao yaliofungwa katika michuano ya kombe la dunia na aliyekuwa mshambuliaji wa Brazil Ronaldo.

KLose alifunga bao lake la kumi na tano dhidi ya Ghana katika mechi iliokuwa na sare ya mabao mawili kwa mawili.

Ghana ilikuwa imechukua uongozi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Ujerumani kabla ya Klose kusawazisha,mda mfupi tu baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada.

Awali timu ya Argentina iliichapa Iran bao moja kwa bila na hivyobasi kufuzu katika michuano ya mchujo.

Nigeria wanapigiwa upato kuingia katika raundi ya mchujo baada ya kuizaba Bosnia Harcegovina bao moja kwa bila na hivyobasi kuwabandua katika mechi hizo.