Ivory Coast nje ya kombe la Dunia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ivory Coast imetupwa nje na Ugiriki

Matumaini ya bara la Afrika kuwakilishwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia huko Brazil yalitumbukia nyong'o Ivory Coast iliyokuwa inahitaji sare tu ilikufuzu kwa mkondo wa pili ikiambulia kichapo cha 2-1mikononi mwa Ugiriki.

Kufuatia ushindi huo Ugiriki ilijikatia tikiti ya mkondo wa pili ambapo sasa itachuana na Costa Rica katika mkondo wa pili

Ugiriki ilikuwa ya kwanza kuweka wazi niya yao kupitia bao la kwanza la Georgios Samaras kunako dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinzi wa Ivory Coast Cheick Tiote kupeana pasi bila ya kuhakikisha usalama wake .

Ivory Coast hata hivyo ilifunga bao la kusawazisha kupitia Wilfried Bony aliyetumia vyema pasi safi kutoka kwa Gervinho.

Haki miliki ya picha v
Image caption Ivory Coast imetupwa nje na Ugiriki

Ivory Coast itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kusonga mbele kwani walipata nafasi nzuri ya kufanya mashambulizi lakini Salomon Kalou akaboronga .

Hata hivyo bao la Ushindi lilitokana na penalti katika muda wa majeruhi baada ya Giovanni Sio kulaumiwa kwa kumtega mshambulizi wa Celtic Georgios Samaras.

Refarii alipuliza kipenga na mshambulizi huyo akafuma mkwaju kimiani mkwaju uliotamatisha ndoto ya Ivory Coast ya kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza .

Ugiriki ilifuzu kama mshindi wa pili katika kundi C na hivyo sasa itakwaruzana na washindi wa kundi D Costa Rica .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Penalti ya Ugiriki iliyozima Ivory Coast

Colombia ilikamilisha mechi za makundi kwa kuiadhibu Japan 4-1 na kuweka rekodi ya kutoshindwa katika makundi.

Colombia itachuana na mshindi wa pili wa kundi D ambaye ni Uruguay baada ya timu hiyo ya Luiz Suarez kuifungisha virago mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia ilipoilaza 1-0.

Kutokana na kichapo hicho Italia iliungana na uingereza kama timu zilizobanduliwa nje baada ya mkondo wa kwanza .

Aidha Afrika kufikia sasa haina mwakilishi katika mkondo wa pili wa kombe la dunia .