Nigeria yafuzu raundi ya pili

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Argentina na Nigeria zimefuzu mkondo wa pili

Super Eagles ya Nigeria ndiyo timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia.

Mabingwa hao wa Afrika walifuzu kama washindi wa pili katika kundi F licha ya kushindwa mabao 3-2 na Argentina katika ya mwisho ya makundi.

Nigeria iliingia katika mechi hiyo ikifahamu fika kuwa iwapo Iran itailaza Bosnia basi wao walifaa kuilaza Argentina.

Hata hivyo Bosnia haikuchelea iliizaba Iran 3-1 na kupunguza shinikizo kwa vijana wa Stephen Keshi .

Nyota wa Argentina Lionel Messi alifunga mabao mawili na kuwasaidia kuibana Nigeria.

Mshambulizi huyo wa Barcelona alifunga bao la kwanza, lakini Ahmed Musa akasawazishia Nigeria chini ya sekunde 80.

Messi alifunga tena kupitia mkwaju wa adhabu na kufanya mambo kuwa 2-1 kabla ya mapumziko, lakini Musa akasawazisha tena.

Marcos Rojo alifunga bao la ushindi kwa Argentina na kuifanya timu yake kumaliza kileleni mwa kundi F kwa kushinda mechi zote tatu walizocheza, huku Nigeria ikifuzu katika nafasi ya pili kwa alama 4 baada ya Iran kushindwa kunyakua alama kutoka kwa Bosnia-Hercegovina.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Argentina na Nigeria zimefuzu mkondo wa pili

Ilichukua dakika 3 tu kabla ya bao la kwanza kufungwa baada ya Messi kukutana na pasi yake Angel Di Maria.

Waargentina hawakuwa wamekamilisha kusherehekea kabla ya Nigeria kusawazisha.

Kiungo cha kati Michel Babatunde alimmegea pasi safi Musa aliyefunga bao hilo la kusawazisha .

Ilikuwa mara ya kwanza kwa historia ya Kombe la Dunia kwa timu mbili zinazochuana kufunga katika dakika tano za kwanza.

Nigeria sasa itachuana Ufaransa katika mkondo wa pili huku