Brazil;Cameroon imeagiza uchunguzi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Biya aagiza Uchunguzi kujua nini kilichangia matokeo duni Brazil

Rais wa Cameroon Paul Biya ameagizi uchunguzi kufanyika kubaini chanzo cha matokeo duni katika kombe la dunia.

The Indomitable Lions ilishindw katika mechi zake zote za makundi mbali na kushuhudia wachezaji wenza wakipigana uwanjani.

Cameroon ililazwa mabao 9 .

Waziri mkuu wa taifa hilo Philemon Yang ameagiza uchunguzi wa kina kubaini chanzo na suluhisho ya matatizo hayo.

Image caption Cameroon ilifungwa mabao 9

Cameroon iliambulia kichapo cha 1-0 dhidi ya Mexico katika mechi yao ya ufunguzi wa kundi A .

Timu hiyo ya Samuel Etoo ilinyeshewa mvua ya mabao 4-0 na Croatia kabla ya kutitimwa mabao 4-1 na wenyeji wa kombe hilo Brazil katika mechi yao ya mwisho.

Alex Song alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kumbo mshambulizi wa Croatia Mario Mandzukic na akapigwa marufuku ya mechi kadhaa na shirikisho la soka duniani Fifa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Assou-Ekotto akimgota Benjamin Moukandjo

Mashabiki wa timu hiyo kote duniani walipigwa na butwaa na kufoka baada ya kushuhudia Benoit Assou-Ekotto akimgota Benjamin Moukandjo.

Kocha Volker Finke alitamaushwa na tukio hilo na kupelekea serikali kutangaza hoja ya kutafuta chanzo na matokeo hayo duni na ya kufedhehesha kwa wa Cameroon.

Suluhisho linapaswa kutangazwa hadharani katika kipindi cha mwezi mmoja.