Ghana na Ureno nje ya Brazil 2014

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ronaldo alifunga bao la ushindi dhidi ya Ghana

Cristiano Ronaldo aliifungia ureno bao la ushindi timu yake ilipoilaza Black Stars ya Ghana 2-1 katika mechi ya mwisho ya makundi.

Kinaya ni kuwa Ureno ilikuwa keshabanduliwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa mechi zao za kwanza.

Ghana itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kusajili ushindi uliohitajika kuihakikishia nafasi katika 16 bora baada ya John Boye alipojifunga mwenyewe.

Asamoah Gyan alifunga bao la kuisawazishia Black stars lakini haikutosha kuifufua kampeini yao kwani walihitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba kuwa Ujerumani ishinde marekani iliwaweze kufuzu kama washindi wa pili katika kundi G.

Ronaldo hata hivyo atamshukuru kipa wa Ghana Fatawu Dauda kwa sifa alizopata baada ya kufunga bao la ushindi kufuatia kipa huyo kumzawadia mpira katika eneo la lango naye akaifuma kimiani.

Image caption Ghana ilikuwa bila Muntari na Boateng ilipochuana na Ureno

Kufuatia ushindi huo wa ureno Ghana ilikamilisha mechi za makundi ikiwa na alama moja pekee huku ureno ikiwa ya tatu na alama 4.

Marekani walijiunga na ujerumani katika mkondo wa pili licha ya Ujerumani kuibana marekani kwa bao moja bila ya jibu.

Ghana hata hivyo ilikuwa tayari inakumbwa na kashfa ambayo wachezaji wake wa kutegemewa Kevin Prince Boateng na Sulle Muntari walitimuliwa kambini huku wale waliosalia wakitishia kususia mechi hiyo ya Ureno kufuatia ubishi kuhusiana na malimbikizi ya marupurupu yao.