Man City yamsajili Fernando wa Porto.

Image caption Mchezaji wa Porto Fernando akimkabili ashley Cole wa Chelsea

Mabingwa wa ligi ya FA nchini Uingereza Manchester City wamemsajili mchezaji wa kiungo cha kati Fernando kutoka kilbu ya Porto kutoka Ureno.

Kilabu hiyo ya Porto ndio iliotangaza makubaliano hayo katika soko la hisa la Lisbon siku ya jumatano baada ya kukubali kumuuza mchezaji huyo kwa takriban paundi millioni 12.

City imethibitisha mpango huo siku ya alhamisi ijapokuwa maelezo ya makubaliano hayo hayakuwekwa wazi.

''Nitacheza uwezo wangu kila ninapokuwa katika uwanja na ninataraji kuichezea kilabu hiyo kwa miaka mingi ijayo.',alisema Fernando.

''Ninafurahia kuwa katika kilabu hii na natamani kucheza katika ligi ya Uingereza''.

Kwa mara ya kwanza mchezaji huyo alihusishwa na timu ya City mnamo mwezi January na ni mchezaji wa pili kusajiliwa na kilabu hiyo baada ya kumsajili beki wa kulia wa Arsenal Bacary Sagna.

''Nina furahi kujiunga na Manchester City'',aliongezea.Najua kulikuwa na mazungumzo ya mimi kusajiliwa na City mnamo mwezi January ,kwa hivyo ninafurahi kwamba makubaliano hayo sasa yameafikiwa na kwamba mimi ni mchezaji wa City.