Mashabiki wa Algeria wazua vurugu

Image caption Mashabiki wa Algeria wazua vurugu Ufaransa

Maafisa wa polisi nchini Ufaransa wamewakamata watu 74 baada ya ghasia kutibuka mashabiki walipokuwa wakishangiliakufuzu kwa Algeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia linaloendelea Brazil.

Watu 30 wametiwa mbaroni katika mji wa Paris baada ya ushabiki kugeuka na kuwa wizi .

Watu wengine 44 walikamatwa katika miji mingine ya Ufaransa .

Ghasia zilitibuka punde baada ya algeria kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Urusi na hivyo The Desert foxes wakajikatia tikiti ya mkondo wa pili kwa mara ya Kwanza .

Image caption Mashabiki wa Algeria wazua vurugu Ufaransa

Mji wa Lyon uliathirika pakubwa maduka kadha yalipovunjwa na mali yenye thamani isiyojulikana kuibiwa.

Maafisa wa usalama wanasema kuwa umati mkubwa wa Wafaransa wenye asili ya Algeria wali waliteketeza moto magari kadhaa mbali na kukabiliana na maafisa wa kulinda usalama .

Msemaji wa wizara ya usalama wa ndani wa Ufaransa Pierre-Henry Brandet alisema kuwa asilimia kubwa ya mashabiki wa Algeria walishangilia bila ya kuvunja sheria lakini baadhi ya wahuni wakatumia fursa hiyo kupora na kuharibu mali ya watu .

Algeria sasa imeratibiwa kuchuana na ujerumani jumatatu ijayo.

Asilimia kubwa ya wachezaji wa Algeria wanaishi Ufaransa .