Raga;Kenya yaishinda Namibia 29-22

Image caption Raga;Kenya imeshinda Namibia 29-22

Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji 15 kila upande ilisajili ushindi mkubwa wa alama 29 -22 katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia huko Madagascar.

Kenya ambayo haijawahi kushiriki wala kuiwakilisha bara la Afrika katika mashindano hayo ya wachezaji 15 kila upande ilikuwa inachuana na Namibia ambayo imeiwakilisha Afrika katika mashindano manne ya kuwania ubingwa wa Afrika katika mchezo wa Raga.

Namibia ambayo kabla ya mechi hiyo ilikuwa imepigiwa upatu kutwaa tiketi hiyo ilisajili alama yake ya kwanza kupitia kwa Heinrich Smit katika dakika 12 ya kipindi cha kwanza .

Nahodha wa zamani wa Kenya Humphrey Kayange akaifungia kenya try ya kwanza muda mchache kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.

kupitia kwa Andrew Amonde aliyefunga try ya ushindi .

Namibia ilirejea uongozini kupitia Try ya Chrysander Botha ambayo Theuns Kotze aliifunga .

Image caption Kenya imeshinda Namibia 29-22 katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la dunia

Kenya ilijifurukuta na kuandikisha Try mbili za haraka kupitia kwa Michael Okombe na Edwin Achayo na kuipa uongozi wa alama 19-12 .

Lavin Asego alifunga penalti huku Amonde akiipa kenya Try ya ushindi .

Katika mechi ya pili ya siku,Zimbabwe iliisambaratisha ndoto ya wenyeji wa mchuano huo Madagascar ya kushireiki kwenye kombe la dunia la raga ilipowanyamazisha alama 57-22 mbele ya mashabiki wa nyumbani 35,000 waliokuwa katika uwanja wa kimataifa wa Mahamasina.

Kila mshiriki wa mashindano haya atacheza mechi tatu miongoni mwa kisha mshindi atajumuika na New Zealand, Argentina, Tonga na Georgia katika kundi C katika fainali za dunia mwakani..

Washindi wa pili kutoka Afrika watakwaruzana na Urusi kisha mshindi kati yao atachuana dhidi ya Uruguay ama Hong Kongkatika kundi A itakayojumuisha Uingereza , Australia, Wales na Fiji.