Algeria:'Ramadhan haikutuangusha'

Image caption Kipa wa Algeria ;Hatukushindwa kwa sababu ya mfungo wa ramadhan.

Kipa wa Algeria Rais M’Bolhi amekanusha madai wachezahi wao walishindwa na Ujerumani kutokana na wao kuwa wadhaifu kwa kufunga saumu.

M’Bolhi ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ambayo Algeria walishindwa mabao 2-1 na Ujerumani katika muda wa ziada anasisitiza kuwa Saumu hakikuchangia kwao Kushindwa.

M’Bolhi anasema kuwa wachezaji hao wamekwisha zoea kucheza hata wakiwa kwenye mfungo na hivyo haipaswi kutolewa kama sababu .

''Tulishindwa katika mechi hiyo mabao mawili bas,

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hatukushindwa kwa sababu ya mfungo wa ramadhan.

Wajua Ramadhan si swala la jumuiya hilo la swala la mtu binafsi na mola wake''alisema MBolhi.

Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na ubishi baada ya kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic kukataa kuulizwa maswali kuhusiana na mfungo wa ramadhan ambao ulikuwa umeanza jumamosi .

Halilhodzic alikataa kufichua idadi ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi .

Halilhodzic, mwenye umri wa miaka 61, alikataa kujibu swali ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.

Image caption Hatukushindwa kwa sababu ya mfungo wa ramadhan.

Kulingana na dini ya Kislamu ,Saumu (Ramadhan) ni nguzo muhimu ya dini na ifikapo wakati wa ramadhan kila mtu mwenye umri wa baleghe hujinyima chakula kuanzia alfajiri hadi magharibi .

Hiyo inaamisha kuw wachezaji wa Algeria hawakuwa wamekula chochote hadi baada ya kipindi cha pili cha mechi hiyo ndipo waliporuhusiwa na dini kunywa na kisha kula .

Kufuatia ushindi huo Ujerumani ilifuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia ambapo watakutana na Ufaransa ijumaa ijayo.