Blatter ayasifu mataifa madogo Brazil

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Blatter na gwiji wa soka Pele

Rais wa shirikisho la soka dunia FIFA Sepp Blatter ameyasifu mataifa madogo kwa kuyaadhibu mataifa ''makubwa''kisoka tena.

Blatter aliyasema hayo katika siku ya mapumziko kabla ya kuanzwa kwa mechi za robo fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

Blatter aliyasema hayo baada ya kubainika kuwa mataifa yote yaliyoshinda makundi yao katika mkondo wa muondoano wa kwanza ndiyo yaliyofuzu kwa robo fainali ya kipute hicho.

Aidha Hii pia ilifungua taswira ambapo timu 4 za bara Ulaya zilifuzu kwa mkondo huo wa robo fainali sawa na 4 kutoka mataifa ya Marekani kusini kinyume na matarajio ya wengi haswa baada ya kushuhudia mataifa yenye sifa kubwa katika kombe la dunia wakiwemo mabingwa wa dunia Uhispania ,mabingwa wa zamani Uingereza na Italia wakibanduliwa nje ya kipute hicho mapema katika raundi ya kwanza.

Kwa sasa hizo ni takwimu na rekodi ambazo zinapaswa kuwachwa katika madaftari ya kumbukumbu Mbivu na mbichi itabainika siku ya ijumaa vigogo wa soka barani Ulaya Ufaransa mabingwa 1998 watakapominyana na washindi wa tatu mwaka wa 2010 Ujerumani.

Mshindi katika mechi hiyo atachuana na mshindi kati ya wenyeji Brazil na Colombia.

Je kunauwezekano wa mataifa ya Marekani kusini kutawala kipute hicho huko Brazil ?

Hilo ndilo swali linalowasumbua wachambuzi wa makala haya ya kombe la dunia .

Majibu ya swali hilo yatapatikana jumamosi mwakilishi wa Marekani Kusini Argentina atakapokwaruzana na mwakilishi wa bara ulaya Ubeljiji.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Costa Rica ni moja ya nchi ambazo zimewashangaza wengi katika michuano ya kombe la dunia Brazil

Hatimaye mechi baina ya Costa Rica na washindi wa pili huko Afrika Kusini ,Uholanzi ndiyo itakayokamilisha vita vya ubingwa wa soka katia ya mabara hayo mawili.

Kihistoria mataifa ya Ulaya ndiyo yamekuwa yakitawala robo fainali za kombe la dunia kuazia mwaka wa 1990.

Hakuna taifa lolote la bara Ulaya ambalo limewahi kushinda kombe la dunia inapoandaliwa Kusini mwa Marekani.

Brazil ndilo taifa la pekee lililowahikutwaa ubingwa wa dunia katika kombe la dunia lililoandaliwa barani Ulaya.

Afrika na Asia na Oceania yamesalia kuwa mashabiki baada ya mataifa wakilishi kubanduliwa nje ya kombe hilo.