Wachezaji wa Ujerumani waugua mafua

Wachezaji saba wa Ujerumani, wanaugua mafua , saa 24 kabla ya mechi yao ya robo fainali dhidi ya Ufaransa.

Kocha Joachim Low anasema kuwa wengi wanaumwa na koo ingawa hakutaja majina ya wachezaji wagonjwa.

"ni mapema sana kufanya uamuzi wowote kuhusu orodha ya wachezaji watakaoingia uwanjani, '' alisema Low

Mats Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema wiki hii huku Mat akikosa mechi ya muondoano dhidi ya Algeria Jumatatu.

Low anaamini kuwa mazingira ya Brazil na safari za hapa na pale nchini humo pamoja na mvua kubwa ndio sababu ya wachezaji wake kuugua.

Lakini aliongeza kuwa , hali sio mbaya sana , sitaki watu wadhani kuwa tunakabiliwa na wakati mgumu, hapana, '' alinukuliwa akisema Low