E.Guinea nje ya CAN 2015.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption E.Guinea nje ya kombe la mabingwa barani Afrika

Equatorial Guinea imeondolewa nje ya mashindano ya kuwania tikiti ya kuwania ubingwa wa Afrika mwakani huko Morocco.

Kamati inayosimamia mchuano huo imeipata taifa hilo na hatiya ya kumchezesha mchezaji kinyume na kanuni za shirikisho la soka duniani FIFA.

Kamati hiyo simamizi iliipata E. Guinea na hatia ya kumshirikisha mzaliwa wa Cameroon Thierry Fidieu Tazemeta, katika ushindi wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya Mauritania tarehe 17 Mei.

Hakuna ushahidi uliotolewa kudhibitisha kuwa Tazemeta alikuwa kabadili Uraiya .

Mauritania ilikuwa imeuliza kudhibitishwa kwa uraiya wa mchezaji huo katika mkondo wa kwanza ilipoibuka mshindi wa 1-0.

Equatorial Guinea hata hivyo ilipuuza madai hayo na ikamshirikisha katika mechi ya pili ambayo E .Guinea iliibuka na ushindi mkubwa wa 3-0 .

Kufuatia kauli hiyo Mauritaniaimerejeshwa mashindanoni na sasa itakabiliana na Uganda katika mkondo wa mwisho wa kufuzu.

Mwaka uliopita Equatorial Guinea ilipoteza mechi mbili kwa sababu sawa na hizo katika mechi ya kufuzu kwa dimba la dunia la Brazil,2014.