Ujerumani imetinga nusu fainali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfungaji bao la Ujerumani

Ujerumani Imesajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali.

Kufuatia ushindi huo dhidi ya Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufuzu kwa nusu fainali katika mashindano manne ya kombe la dunia mfululizo .

Ujerumani ndiyo timu ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

Kufuatia ushindi huo Ujerumani watakutana na mshindi baina ya Brazil na Colombia katika hatua ya nusu fainali .

90'30 Ujerumani 1-0 Ufaransa

85:35 Ujerumani 1-0 Ufaransa

58:50 Kadi ya kwanza ya manjano inamwendea Sami Khedira refarii Nestor Pitana amechoshwa na mchezo wake wa ngware .

57:34 Depsome Elisha Kahama tz! Ujeruman bingwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bao la Mat Hummels

Samwel Paul: Ufaransa lazima watoke hata kupambana kwao kote Ujerumani

51:30Husein Mono Wa Mwanga Kilimanjaro TZ ;Ufaransa bado wanna uwezo hata was kushinda!

45:20 Kipindi cha pili kimeanza

45'' Kipindi cha kwanza kimekamilika .

44 Ujerumani 1-0 Ufaransa

41 Benzema anakosa fursa nyengine ya kuisawazishia Ufaransa.

40'' Mechi hii inaendelea katika uwanja wa kihistoria wa Maracana

Kufikia sasa Bao la dakika ya 12 la Mats Hummels ndilo linaipatia ujermani kipao mbele

Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi kati ya Brazil na Colombia katika nusu fainali.

Ujerumani inakabiliana na Ufaransa kutafuta tikiti ya nusu fainali ya kombe la dunia .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wa Ufaransa