FIFA huenda ikaiadhibu Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption FIFA huenda ikaipiga marufuku Nigeria kwa kuingilia usimamizi wa kandanda.

Shirikisho la soka duniani FIFA huenda ikaichukulia hatua kali Nigeria kwa kuingilia kati usimamizi wa kandanda.

Mabingwa hao wa Afrika huenda wakapigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda baada ya mahakama nchini humo kufuta kaziafisi yote ya shirikisho la soka nchini humo

Waziri wa michezo wa Nigeria Tammy Danagogo alimteua Lawrence Katiken kuwa msimamizi mkuu wa NFF.

Dukuduku nchini humo zinasema kuwa matokeo duni ya timu hiyo hayakusaidia hali mbaya ya uhusiano na serikali ya nchi hiyo.

Super Eagles iliambulia kichapo cha 2-0 mikononi mwa Ufaransa katika raundi ya pili ya kombe la dunia na hivyo kufungashwa virago.

Mahakama ya jimbo la Plateau ilitoa amri ya kupinga uongozi wa Aminu Maigari, na kamati yake nzima.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption FIFA huenda ikaipiga marufuku Nigeria kwa kuingilia usimamizi wa kandanda.

Matukio kama hayo katika miaka ya awali yalisababisha marufuku ya FIFA kwa Nigeria sawa na Kenya.

Nigeria ilinusurika kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwaka wa 2010 baada ya serikali kutishia kususia mashindano yote kwa miaka miwili kwa niya ya kuijenga upya kikosi chake kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia Afrika Kusini..

Nigeria ilifuzu kwa hatua ya pili huko Brazil kwa mara ya tatu katika historia ya mashindano ya kombe la dunia .

Nigeria ilikuwa imewahi kufuzu kwa kombe a dunia katika miaka ya 1994 na 1998.

Mwaka uliyopita Nigeria ilitawazwa mabingwa wa Afrika huku kikosi chake cha vijana wasiozidi umri wa miaka 17 wakishinda kombe la dunia .