Liverpool kumnunua Origi na Markovic

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Liverpool kumnunua Origi na Markovic na kumuuza Suarez

Liverpool ya Uingereza imekubaliana na klabu ya Lille kumsajili mshambulizi wa Ubeljiji ambaye ni mzaliwa wa Kenya Divock Origi .

Timu hiyo vilevile inapania kumsajili kiungo cha kati wa Serbia na Benfica Lazar Markovic .

The Reds wamekubalia kutoa kitita cha pauni milioni £10m kwa tineja huyo 19 Origi.

Origi hata hivyo anatarajiwa kukamilisha mazungumzo juma lijalo .

Klabu hiyo vilevile inapania kukamilisha makubaliano na Markovic, ambaye ataigharimu takriban pauni milioni £25m.

Image caption Liverpool kumnunua Origi na Markovic na kumuuza Suarez

Mazungumzo ya wawili hao yanawadia huku ikifahamika kuwa Liverpool inatarajia kumuuza mfungaji mabao mengi katika msimu uliopita katika ligi ya Uingereza Luis Suarez, kwa Barcelona kwa pauni milioni £75m.

Barca imeonesha niya ya kumnunua Suarez fauka ya matatizo yaliyokumba baada ya kumngata mlinzi wa Italia Chiellini katika mechi ya kombe la dunia .

Liverpool vilevile inamtaka Alexis Sanchez, katika uhamisho huo wa Suarez .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suarez anahamia Barcelona

Liverpool tayari imewanunua Rickie Lambert,32, kiungo Adam Lallana ,kutoka Southampton kwa gharama ya pauni ya milioni £29m.

Emre Can,20, vilevile ameshadunda Anfield.

Kocha Brendan Rodgers anatafuta kuimarisha kikosi chake kabla ya kushiriki mchuano wa kuwania ubingwa wa bara uropa mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopitanyuma ya Manchester City.