Luiz awaomba radhi mashabiki

Image caption Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani

Nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa timu hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao ilipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

Amini Usiamini Ujerumani ilikuwa inaongoza mabao 5-0 kufikia dakika 29 ya kipindi cha kwanza .

"Wajerumani walikuwa timu bora zaidi yetu''

Luiz,ambaye alitajwa kama nahodha wa muda baada ya marufuku ya Nahodha Thiago Silva kumlazimu kutizama tu mechi hiyo alisema hawjui kilichotendeka lakini ni wakati wao kujifunza kutokana na aibu hiyo ya kusakamwa 7-1. "Ni siku ya majonzi tele kwa wabrazil''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Luiz akilia baada ya kushindwa na Ujerumani

"Mtuwieni radhi sijui tutafanya nini ilituwaone tena wabrazil wakitabasamu,?

Kilio kimezidi kote nchini humo haswa baada ya nyota wa Brazil Neymar kujeruhiwa uti wa mgongo Ijumaa iliyopita katika mechi ya kufuzu kwa nusu fainali dhidi ya Colombia.

Kwa Upande wake Kipa wa Brazil Julio Cesar alitaja dakika hizo kumi timu hiyo ilipofungwa mabao manne kuwa sawa na kuzimia.

''Sio jambo unaloweza kujieleza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Julio Ceasar; Ujerumani ilikuwa timu bora

Kombe hili la dunia limekuwa lenye ufanisi hadi leo.

Hata hivyo tunawashukuru Wabrazil kwa kutuunga mkono katika kipindi hichi chote .

Hata wachezaji wakiomba msamaha kwa kichapo hichi cha leo ,ni wazi kuwa mjerumani alituzidi maarifa .

Lazima tukali hilo walikuwa bora kutuliko leo.'''