'Kimbunga' cha magoli chapiga Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafungaji mabao ya Ujerumani

Ujerumandiyo timu ya kwanza kufuzu kwenye Fainali ya kombe la dunia Brazil 2014, baada ya kuinyeshea wenyeji Brazil mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo Horizonte.

Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.

Kabla ya mechi hiyo vyombo vya habari vilikuwa vimemulika mfumo wake Luiz Felipe Scolari vikidai alikuwa ameumba timu yake kumtegemea Neymar.

Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.

Je Scolari atasingizia nini ?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Fernandinho akiuhuzunika baada ya kutingwa bao la 5 na Ujerumani

Ilikuwa wazi tofauti ya mbinu za makocha hao wawili wajerumani walipoanza kwa kuwashirikisha washambulizi Miroslav Klose,Thomas Muller na Mesut Ozil huku Schweinsteigerakiwaongoza Toni Krooos Khedira na Lahm katika kiungo cha Kati.

Na Baada ya nipe nikupe ya kufungua mechi Iliwachukuwa Wajerumani takriban dakika kumi tu za kwanza kupenya safu ya ulinzi ya Brazil iliyokuwa inakosa uzoefu wa Thiago Silva.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kilio kimetanda Brazil.

Thomas Muller alifungua kivuno hicho cha mabao kabla ya Klose kuidhibitishia Ujerumani fainali yao kombe la dunia kwa mkwaju uliomwacha kipa wa Brazil Julio Cesar asijue la Kufanya.

Klose kwa ushirikiano na Toni Kroos walifunga bao la tatu na la nne katika kipindi cha dakika moja.

Sami Kheidira alifunga la tano kunako dakika ya 29 kabla ya mchezaji wa akiba Andre Schurrle kufunga mabao ya 6 na ya 7 .

Bao la kufutia machozi la Brazil lilifungwa na Oscar kunako dakika ya mwisho ya mechi hiyo.

00:90 Oscar anaiifungia Brazil bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya mechi hii ya kihistoria .

00:70 Andre Schurrleanafanya mambo kuwa 6-0 kwa Ujerumani.

00:70 GOOOOOOOAL

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Julio Cesar haamini dunia imempasukia wapi .

00:60 Ujerumani 5- Brazil

00:59 Miroslav Klose anapumzishwa Andre Schurrle anaingia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bao la Milaslav Klose

00:58 Brazil inaendelea kutafuta angalau bao la kufutia machozi lakini Nuer hapishi

00:57

00:54' Kipa Manuel Nuer anainyima brazil bao la kufutia machozi

23:35

23:30 Ujerumani 5-0 Brazil

23:26

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ujerumani 1-0 Brazil

23:26 Toni KROOOOOS

23:24 GOOOOOOAL !Toni KROOOOS

23:20 Thomas Muller anafunga bao la pili la Ujerumani

23:20 GOOOOOOAL

23:20 Ujerumani 2-0 Brazil

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bao la Muller

Ujerumani hawajawahi kushindwa katika mechi ambayo wametangulia kufunga.

23:18 Brazil wanaonekana wameduwazwa na bao hilo la Muller

23:15 Kona kuelekea upande wa Ujerumani

23:11 Ujerumani 1-0 Brazil

23:10 Thomas Muller anaiweka Ujerumani mbele 1-0

23:10 GOOOOOOOOOAL

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Muller akishangilia bao lake

23:10 Kona kuelekea lango la Brazil.

23:09 David Luiz analazimika kufanya kazi ya ziada kufuatia mashambulizi ya mjerumani

23:05 Ujerumani inashambulia lango la Brazil lakini wapi inazimwa .

23:02 Ujerumani 0-0 Brazil

23:01 Ujerumani haina matatizo ya wachezaji ikilinganishwa na Scolari ambaye amelazimika kuchezesha kikosi bila ya Neymar

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Timu ya Ujerumani

23:00 Mechi Imeanza

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Timu ya taifa ya Brazil itakavyokuwa katika mechi hii bila ya Neymar

22:57

22:55 Wimbo wa taifa wa Brazil unapigwa hapa uwanjani ,,mashabiki wa Brazil wanaimba

22:54 Wimbo wa taifa wqa Ujerumani unachezwa hapa mbele ya uwanja uliofurika furifuri

22:52Mashabiki wa Brazil na wale wa Ujerumani wakishangilia timu zao kabla ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Brazil inachuana Ujerumani

22:50

22:50Wenyeji wa kombe la dunia Brazil wanachuana na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali.